Afrika, ikiwa ni pamoja na Tanzania, imefaidika sana na maendeleo na ushirikiano wa China tangu kuanzishwa kwa China Mpya miaka 75 iliyopita, Joseph Kahama, katibu mkuu wa Jumuiya ya Kukuza Urafiki kati ya Tanzania na China, aliiambia Xinhua kabla Siku ya Kitaifa ya China.
Tangu kuanzishwa kwake mnamo Oktoba 1, 1949, Jamhuri ya Watu wa China imeonyesha mifano bora kwa Tanzania, Afrika na dunia kupitia mafanikio ya ajabu katika kupunguza umaskini na kudhibiti magonjwa ya milipuko kama vile COVID-19, miongoni mwa mafanikio mengine makubwa.
“China imewaondoa karibu watu milioni 800 wa vijijini kutoka kwenye umaskini. Haya ni mafanikio makubwa katika kipindi kifupi sana cha miaka 75,” alisema na kuongeza kuwa China imewaondoa watu wengi kutoka kwenye umaskini huku ikiendelea kuzisaidia nchi zingine kujiendeleza.
Kahama alibainisha kuwa katika kipindi cha miaka 75 iliyopita, China imekuwa nchi ya pili kwa uchumi mkubwa duniani.