TAWA YAMDHIBITI MAMBA ALIYEZUA TAHARUKI BUCHOSA

Kijiji cha Kahunda charindima Kwa nderemo na vifijo

Na. Beatus Maganja

Maofisa wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Nchini – TAWA kwa kushirikiana na wananchi wa Kijiji cha Kahunda kilichopo Kata ya Katwe Halmashauri ya Buchosa wilayani Sengerema na mkoa wa Mwanza wamefanikiwa kumdhibiti mamba aliyezua taharuki takribani wiki nzima Kijijini humo kabla ya kuleta madhara Kwa binadamu.

Tukio la kumdhibiti mnyama huyo mkali na mharibifu lilitokea oktoba 03, 2024 mara baada ya wananchi wa Kijiji hicho kutoa taarifa kwa Maofisa wa TAWA Kanda ya ziwa kituo kidogo cha Mwanza ambao walifika haraka eneo la tukio na kufanikiwa kumdhibiti mnyama huyo Kwa kumuua Kwa mujibu wa Sheria.

Mamba
Maafisa wa wanyamapori wakimwangalia mamba

Wananchi wa Kahunda wamesema mamba huyo amekuwa akileta taharuki takribani wiki nzima Kwa kukamata mifugo yao wakiwemo bata, kuku na mbwa Katika mwalo wa Kijiji hicho na Kijiji cha zabaga hali ambayo ilikuwa ikiwafanya waishi Kwa wasiwasi mkubwa na kushindwa kufanya shughuli za kibinadamu Kwa amani katika ziwa hilo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kahunda Bw. Athumani Wambura ameipongeza Serikali kupitia maofisa wa TAWA kwa kufanikisha zoezi la kumdhibiti mamba huyo na jitihada zote zinazofanywa na taasisi hiyo Kijijini humo ikiwa ni pamoja na hatua mbalimbali wanazochukua Katika kulinda maisha ya wananchi wa wilaya ya Sengerema dhidi ya athari za wanyamapori wakali na waharibifu hususani mamba na viboko.

“Niseme tu nawapongezeni sana hawa ndugu zangu wa maliasili (TAWA) jambo walilolifanya ni kubwa kwa wananchi wetu, Kwa namna moja au nyingine tumepata amani kwa kumdhibiti huyu mnyama ambaye ni tishio kubwa sana. Kwa miaka ya hivi karibuni wanyama hawa wameweza kuua watu wetu zaidi ya watatu katika Kijiji cha Kahunda” amesema
Athumani Wambura

Kwa upande wake Afisa habari wa TAWA Beatus Maganja amewapongeza wananchi wa Kijiji hicho Kwa ushirikiano walioutoa mpaka kufanikisha zoezi la kumdhibiti mamba huyo na kuwataka waendelee kuchukua tahadhari wanapofanya shughuli zao Katika ziwa hilo pamoja na kuzingatia elimu inayotolewa na watalamu hao huku akiwahakikishia kuwa Serikali imetenga fedha Kwa ajili ya kuongeza vizimba viwili.

Related Posts

Update: Urgent search for dad missing with six-month-old baby son

A search has been launched for a dad and his six-month-old baby son after they were last seen yesterday afternoon. Adam Skindzier, 44, was with his son Nathan in the Netherton…

Read more

Trump surrounded toilet rolls and nappies during Hurricane Helene aid speech

Ex-President Donald Trump’s latest move touting the Hurricane Helene relief efforts of fellow Republicans had him standing next to a mound of toilet paper rolls and nappies. Trump appeared next to Georgia Governor…

Read more

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You Missed

Eggs Production

Eggs Production

Update: Urgent search for dad missing with six-month-old baby son

Update: Urgent search for dad missing with six-month-old baby son

Trump surrounded toilet rolls and nappies during Hurricane Helene aid speech

Trump surrounded toilet rolls and nappies during Hurricane Helene aid speech

Hurricane Kirk set to bring snow, heavy rain and strong winds to the UK 

Hurricane Kirk set to bring snow, heavy rain and strong winds to the UK 

Update: Man stabbed to death in block of flats in east London

Update: Man stabbed to death in block of flats in east London

How Michael Schumacher communicates after F1 legend is ‘seen in public’

How Michael Schumacher communicates after F1 legend is ‘seen in public’